JINSI YA KUTUMIA BANDO LAKO KIUFASAHA
Habari yako mpendwa msomaji wa nakala hii,natumai u mzima wa Afya lakin pia pole na majukumu mbalimbali uliyonayo.
Siku za hivi karibuni kumekuwa na malalamiko juu ya matumizi ya Data zetu"Bando''. Baadhi ya watu wamenukuliwa kwa kusema, baadhi ya makampuni yanaiba bando zetu. Lakini, ukweli ni kwamba, makampuni ya simu hayahusiki katika hili bali ni matumizi na mipangalio ya vifaa vyetu vya mawasiliano tunavyotumia.
Katika kufahamu ilo, mwandishi chipukizi 'Daniel liwowo Malachite' ' anakuletea mbinu mbalimbali zitakazo weza kukusaidia kutumia bando lako angalau kwa muda mrefu kidogo tofauti na zamani.
Vifaa vingi ambavyo tunavitumia vya mawasiliano hasa simu na Computer vinauwezo wa kutumia data zetu bila ya sisi kufahamu yaani '' Background usage '' na ndiyo sababu moja wapo ya bando zetu kuisha kwa haraka. Sababu nyingine pia ni kasi kubwa ya Internet kuliko matumizi yetu, mfano mtu anatumia kasi ya 4G wakati anatumia kuangalia picha Facebook.
Leo tutaongelea jambo ilo la kwanza ambalo ni '' Background data usage ''. Huu ni mfumo ambao Applications nyingi hutumia ambapo zinatumia data bila wewe kufahamu na ata wewe bila kuzitumia.
JINSI YA KUZUIA BACKGROUND DATA USAGE.
Zifuatazo ni baadhi ya njia rahisi unazo weza kuzuia matumizi hayo ya Background,
1.Chagua Application ambayo umekua huitumii mara kwa mara, mfano, wewe sio mtumiaji sana wa YouTube ivyo unaweza kuichagua.
2.Bonyeza iyo Application kama unataka kuiunstall, kisha chagua '' Application Information''.
3.Chagua' 'Data usage, kisha utaona sehemu imeandikwa' 'Background data' kisha utaona mshale rangi ya blue(huweza kuwa tofauti na kuwa na rangi nyingine kulingana na simu) kisha gusa iko kishale na kitarudi mpaka mwanzo kabisa.
3.Hongera,umefanikiwa kuzuia background data usage,unaweza kutoka kwa kugusa 'home bottom '
Pia, utaendelea kufuata hayo maelekezo kwa kila App ambayo utakua huitumii mara kwa mara.
FAIDA ZA KUZIMA BACKGROUND DATA USAGE.
1.Data huweza kukaa kwa muda mrefu, hiii ni kutokana na data hutumika kutokana na Applications unazotumia.
2.Huepusha simu kushika joto kali ''Over heating' '
MADHARA YA KUZUIA BACKGROUND DATA USAGE.
Madhara yake ni kuwa, hutaweza kupata taarifa endapo kama hutoitumia Applications izo, kwasababu Applications izo zimezimwa uwezo wa kutoa taarifa wakati kuzitumii.
Nakala hii imeandaliwa na Daniel de malachite.
Asante kwa kupitia nakala hii, natumai umepata kitu cha kujifunza, karibu tena ili uzidi kujifunza kila siku🙏
Comments
Post a Comment
Anyone