Posts

JINSI YA KUTUMIA BANDO LAKO KIUFASAHA

Habari yako mpendwa msomaji wa nakala hii,natumai u mzima wa Afya lakin pia pole na majukumu mbalimbali uliyonayo.  Siku za hivi  karibuni kumekuwa na malalamiko juu ya matumizi ya Data zetu"Bando''. Baadhi ya watu wamenukuliwa kwa kusema, baadhi ya makampuni yanaiba bando zetu. Lakini, ukweli ni kwamba, makampuni ya simu hayahusiki katika hili bali ni matumizi na mipangalio ya vifaa vyetu vya mawasiliano tunavyotumia. Katika kufahamu ilo, mwandishi chipukizi 'Daniel liwowo Malachite' ' anakuletea mbinu mbalimbali zitakazo weza kukusaidia kutumia bando lako angalau kwa muda mrefu kidogo tofauti na zamani.      Vifaa vingi ambavyo tunavitumia vya mawasiliano hasa simu na Computer vinauwezo wa kutumia data zetu bila ya sisi kufahamu yaani '' Background usage '' na ndiyo sababu moja wapo ya bando zetu kuisha kwa haraka. Sababu nyingine pia ni kasi kubwa ya Internet kuliko matumizi yetu, mfano mtu anatumia kasi ya 4G wakati anatumia kuangalia picha ...